Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, ambayo ni fursa ya kutambua na kuadhimisha mchango wa wanawake katika jamii zetu. Ni siku ya kuenzi nguvu, ujasiri, na uvumilivu wa wanawake ulimwenguni kote, wakiwa kama wauguzi, waalimu, wajasiriamali, viongozi, na walinzi wa utamaduni wetu. Kupitia jitihada zao, wanawake wameleta mabadiliko chanya katika jamii zetu.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya, “Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii,” inatuhamasisha kuelewa umuhimu wa kuwezesha wanawake kushiriki katika ngazi za kufanya maamuzi, uongozi, na usawa wa kijinsia ili kufikia maendeleo endelevu. RC Chalamila amesisitiza kwamba maadhimisho haya yanalenga kuelimisha, kuhimiza, na kuhamasisha umma kuhusu umuhimu huu.
Ahsanteni kwa kujitolea na kuwa nguzo imara katika kujenga jamii bora. Siku ya Wanawake Duniani iwe njema kwenu nyote! Tufanye kazi kwa pamoja kuleta mabadiliko chanya na kuendelea kutetea usawa na haki kwa wanawake ulimwenguni kote.